Mfuko unalenga zaidi wale wajasiriamali wa kati ambao huongeza thamani kwenye bidhaa za kilimo na wenye mahitaji ya kifedha ya muda mfupi na mitaji ya muda wa kati na mrefu. 
Pamoja na kutoa mikopo ili kukuza biashara yako, sisi pia tunakusaidia kuongeza ufahamu wa kina katika biashara yako. Kukuwezesha kifedha pamoja na utambuzi wa kina kuhusu jinsi ya kukuza biashara yako, kutapelekea biashara yako kuwa mahiri na hatimaye kuongeza kipato zaidi mfukoni mwako. Bidhaa za kifedha zinazozotolewa kwa niaba ya mfuko wa SME Impact Fund ni zifuatazo:

Mikopo ya ununuzi wa pembejeo
inawalenga wazindikaji wanaotarajia kuwapa pembejeo wakulima waliongia nao kilimo cha mikataba. Hizi pembejeo za kilimo ni kama vile mbegu, mbolea na dawa, hasa wale wanaofanya kilimo cha mkataba na wakulima. Mikopo hii italipika kati ya miezi mitatu hadi mwaka mmoja.

Mikopo ya ununuzi wa mazao
ni aina ya mikopo kwa ajili ya kununua mazao ya kilimo au bidhaa za msimu au malighafi wakati wa kipindi cha mavuno. Mikopo inaweza kutumiwa kununua mazao kama mahindi, pamba, katani, mbegu za mafuta, chai, kahawa n.k. Pia bidhaa za sekta ndogo ya matunda na mbogamboga (k.m. maharage, nyanya, machungwa, maembe n.k. Mikopo hii italipika katika muda mfupi zaidi kuliko ya pembejeo kwani mzunguko wake ni mfupi pia.

Mikopo kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kilimo na miundo mbinu:
kopo huu ni kwa ajili ya kuwawezesha wateja kuwekeza kwenye vifaa muhimu vya kuboresha mashamba yao (plau, umwagiliaji, zana za mikono, nk). Pia kuwekeza kwenye mitambo ya kupimia ubora, mashine za kusafisha au kukaushia bidhaa. Mikopo hii inaweza pia kulipia gharama za mafunzo ya kilimo bora. Urejeshaji wa mikpo ya aina hii hauzidi miaka mitatu.

Mikopo kwa ajili ya uwekezaji kwenye kiwanda au kampuni:
Mkopo hii ni kwa ajili ya kuwekeza kwenye kiwanda chako au kampuni ili kuongeza na kuboresha uwezo na ufanisi kupitia kununua zana mbalimbali kama mashine, maghala au vitendea kazi muhimu. Kampuni zinaweza kukopa kwa ajili ya kununulia mali zisizohamishika kama ardhi, mashamba, na mitambo ya kiwandani. Pia mikopo hii inaweza kuwa kwa ajili ya leseni, usajili kwenye viwango vya kimataifa kama HACCP, GLOBALGAP, kilimo hai n.k. Mikpo hii italipika katita muda usiozidi miaka mitano.