Tunaamini katika upekee wa bidhaa zetu za kifedha na ushauri kwenye kukidhi mahitaji ya biashara yako. Sisi hufanya hivi kupitia mikopo kwa wajasiriamali wa kati ya:
• Ununuzi wa mazao: Mkopo kwa ajili ya kununua mazao ya kilimo au bidhaa za msimu au malighafi wakati wa kipindi cha mavuno.
• Ununuzi wa pembejeo: Mkopo kwa ajili ya kusaidia wateja wako kununulia pembejeo za kilimo kama vile mbegu, mbolea na dawa, hasa wale wanaofanya kilimo cha mkataba na wakulima.
• Uwekezaji kwenye kiwanda au kampuni: Mkopo kwa ajili ya kuwekeza kwenye kiwanda chako au kampuni ili kuongeza na kuboresha uwezo kupitia kununua zana mbalimbali kama mashine, maghala au vitendea kazi muhimu
• Ununuzi wa vifaa vya kilimo na miundo mbinu: Mkopo kwa ajili ya kuwawezesha wateja wako kuwekeza kwenye vifaa muhimu vya kuboresha mashamba yao (plau, umwagiliaji, zana za mikono, nk)