Mfuko unayo nyenzo mahsusi ya kuchambua mahitaji ya kifedha ya mteja mtarajiwa. Kabla ya kuyapeleka maombi ya mteja kwa ajili ya ushauri wa Kamati ya Mikopo, tathimini ya kina huwa inafanywa ya mjasiriamali na biashara yake. Mara mkopo ukishapitishwa na fedha kutolewa kwa mteja, wafanyakazi wa Match Maker Fund Management huwa wanafanya kila jitihada ili mteja afanikishe ndoto yake na aweze kulipa mkopo. Ingawaje Match Maker Fund Management ni kampuni changa bado, inakuwa kwa haraka sana. Matarajio yake ni kutoa fursa ya mikopo kwa wajasiriamali wa kati ndani na nje ya Tanzania, kwa kupitia mfuko huu, na baadaye kwa kusimamia mifuko mingine.